Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni jana Alkhamisi, Abdul-Malik al-Houthi alisema kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni ambayo yanafanywa kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, wakazi wengi wa Ukanda wa Gaza wameyakimbia makazi yao.
"Marekani inaunga mkono kuhamishwa kwa lazima kwa watu wa Gaza, na Wazayuni wamekiri kwamba Marekani imewapa uhuru kamili kuhusiana na Ukanda wa Gaza," amesema.
"Adui Mzayuni, akiungwa mkono na Marekani, anaendeleza uchokozi wake wa kikatili dhidi ya Gaza, kuwamiminia mabomu wakimbizi, na licha ya kuharibu sekta ya afya, anaendelea kulenga vituo vya matibabu, kama ilivyotokea katika Hospitali ya al-Ma'madani."
Al-Ma'madani au al-Ahli Arab ilikuwa hospitali ya mwisho kufanya kazi huko Gaza, iliyopigwa na makombora mawili ya Israeli; mashambulizi hayo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, yalitoa "pigo kubwa kwa mfumo wa afya ambao tayari umesambaratishwa katika Ukanda huo" siku ya Jumapili.
Hii ni katika hali mbayo, jana Alkhamisi, jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya bandari ya mafuta ya Ras Isa magharibi mwa Yemen, na kuua wafanyakazi na wahudumu wa afya karibu 40, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa.
Serikali ya Yemen imeapa kwamba, uhalifu huu hautapita bila kujibiwa, ikisisitiza kuwa Marekani haitaambulia chochote ila kushindwa na kufeli kwa fedheha.
342/
Your Comment